Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-RWANDA-Diplomasia

Afrika Kusini na Rwanda zimo mbiyoni kuboresha uhusiano wao

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma (kushoto) akiwa na rais wa Rwanda, Paul Kagame (kulia).
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma (kushoto) akiwa na rais wa Rwanda, Paul Kagame (kulia). Kongo TIMES
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Mkutano wa kikanda uliyoandaliwa jana katika mji mkuu wa Angola, Luanda umejaribu kuweka sawa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Afrika Kusini na Rwanda, uhusiano ambao ulififia kwa siku kadhaa tangu Afrika Kusini ilipowafukuza wanadiplomasia wa Rwanda mjini Pretoria na Rwanda kujilipiza kisase kwa kuwafukuza wanadiplomasia wa Afrika Kusini mjini Kigali. 

Matangazo ya kibiashara

Afrika Kusini ilichukua uamzi wa kuwafukuza wanadiplomasia wa Rwanda, baada ya makaazi ya mkuu wa zamani wa majeshi nchini Rwanda, Kayumba Nyamwasa, aliyekimbilia katika mji wa Johannesburg kushambuliwa na watu wasiyojulikana.

“Katika mkutano wa kikanda, kumezungumzia uhusiano wa kidiplomasia kati ya Afrika Kusini na Rwanda, na makubaliano yameafikiwa, kusema kwamba mataifa haya mawili yanapaswa kuketi pamoja kwenye meza ya mazungumzo na kupata suluhu maridhawa”, imesema ikulu ya Afrika Kusini katika tangazo iliyotoa.

Rais Jacob Zuma ametangaza kwa mara ya kwanza kuhusiana na hali hio kwenye radio moja ya Afrika Kusini iitwayo Safm kwamba nchi yake ina haki ya kumlindia usalama mkimbizi wowote, hususan Faustin Kayumba Nyamwasa, mkuu wa zamani wa majeshi ya Rwanda, ambaye makaazi yake yalishambuliwa mwanzoni mwa mwezi wa machi.

“Nimezungumza na rais Paul Kagame kwamba tuko tayari kupeana taarifa za kina na kupata jawabu ya swala hilo”, amesema Jacob Zuma.

“Rwanda inadhani kwamba, wakimbizi wa Rwanda wamekua wakipanga namna ya kuhatarisha usalama nchini humo, na sisi tunapaswa kuheshimu majukumu ya kimataifa wakati watu wanaingia nchini chini ya uvuli wa ukimbizi, kuna mkataba uliyoafikiwa ili mataifa haya yakutane, na tumekubaliana kwa hilo”, amesma Zuma.

Afrika Kusini iliwafukuza wanadiplomasia wanne kutoka Rwanda, na mmoja kutoka Burundi, Kigali kwa upande wake iliwafukuza wanadiplomasia sita kutoka Afrika Kusini.
Afrika Kusini imebaini kwamba, baada ya uchunguzi ilibainika kwamba wanadiplomasia waliyofukuzwa walihusika katika mashambulizi dhidi ya makaazi ya Faustin Kayumba Nyamwasa.

Faustin Kayumba Nyamwasa aliponea katika jaribio la kuuawa kwa risase mjini Johannesburg juni mwaka 2010, ambapo watuhumiwa bado wanasikilizwa na mahakama ya Afrika Kusini.

Hivi karibuni mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi ya Rwanda, Patrick Karegeya, alikutwa alinyongwa januari mosi katika hoteli ya mjini Johannesburg.

“Matukio hayo yanahusiana na hali ya kisiasa inayojiri nchini Rwanda, na yametokea nchini mwetu”, ilibaini Afrika Kusini katikati ya mwezi mchi, ikisema kwamba hali hio ni jaribio la kuhatarisha usalama wa taifa.
 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.