UKRAINE-URUSI-Diplomasia

Hali ya hatari inaendelea kutanda Ukraine

Wanaharakati wanaounga mkono Urusi wakiandamana mbele ya jengo la serikali katika jimbo la mashariki la Kharkiv, aprili 7 mwaka 2014.
Wanaharakati wanaounga mkono Urusi wakiandamana mbele ya jengo la serikali katika jimbo la mashariki la Kharkiv, aprili 7 mwaka 2014. REUTERS/Stringer

Polisi nchini Ukraine imewakamata watu 70 ambao wanaunga mkono nadharia ya Urusi waliyokuwa wamedhibiti jengo la serikali katika mji wa Kharkiv, mashariki mwa Ukraine, afisa mmoja wa wizara ya mambo ya ndani wa Ukraine amefahamisha.

Matangazo ya kibiashara

Wanaharakati wanaounga mkono harakati za Urusi, ambao walivamia jana jengo hilo la serikali, na baadae wakaondoka usiku baada ya mazungumzo. Wakati huo waziri wa mambo ya ndani, Arsen Avakov, aliwasili sehemu hio na kuwataka raia hao kuachana na tabia ya kuvamia majengo ya serikali. Lakini hali ya mvutano iliendelea kushuhudiwa siku nzima ya jana, huku maelfu ya waandamanaji wakiwa walikusanyika mbele ya jengo hilo la serikali.

Upande mwengine idadi ndogo ya wanaharakati wanaounga mkono ushirikiano wa Ukraine na Ulaya wameonekana wakiandamana pia pembezuni mwa jengo la serikali.
Waandamanaji wanaounga mkono Urusi waliwasha moto baadhi ya ofisi za serikali, kulingana na taarifa iliyotolewa na maafisa wa wizara ya mambo ya ndani, lakini moto huo ulizimwa haraka.

Baada ya matukio hayo, polisi ilifanya operesheni dhidi ya ugaidi iliyopelekea jengo la serikali linalindwa vilivyo, na watu 70 walikamakatwa katika operesheni hio, wamefahamisha maafisa hao wa wizara ya mambo ya ndani.

Maafisa hao wamebaini kwamba hakuna risase liliyofyatuliwa.

Waziri wa mabo yandani wa Ukraine, ameandika jana usiku kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba: “operesheni dhidi ya ugaidi imeanza. Maeneo ya katikati ya mji yamezingirwa. Msiwe na hofu”.

Mbunge mmoja ajulikanaye kwa jina la Nikolaï Kniajitski, ambaye amezungumza jana na Avakov, amesema kupitia ukurasa wake wa Facebook kwamba operesheni hiyo imeendeshwa na kikosi maalum kinachomilikiwa na wizara ya mambo ya ndani, kiitwacho “Jaguar”.

Hayo yakijiri wizara ya mambo ya kigeni ya Urusi imefahamisha leo asubuhi kwamba Ukraine imewatuma wanajeshi wake ili kukabiliana na wanaharakati waliyojitenga na Ukraine, na kutahadhari kwamba huenda kuatokea vita vya wenyewe kwa wenyewe.