NORWAY-RWANDA

Serikali ya Norway kumrejesha nchini Rwanda Eugène Nkuranyabahizi anaeshukiwa mauaji ya kimbari

Siku moja baada ya kuanza maadhimisho ya mauwaji ya kumbukumbu nchini Rwanda, Mahakama nchini Norway imeamua kumtu Rwanda Eugène Nkuranyabahizi.
Siku moja baada ya kuanza maadhimisho ya mauwaji ya kumbukumbu nchini Rwanda, Mahakama nchini Norway imeamua kumtu Rwanda Eugène Nkuranyabahizi. REUTERS/Noor Khamis

Vymbo vya sheria nchini Norway vimeruhusu kutumwa nchini Rwanda kwa Eugène Nkuranyabahizi, ambaye anatuhumiwa kuhusika katika mauwaji ya kimbari yaliyotokea mwaka 1994 katika taifa hilo ndogo la kanda ya maziwa makuu.

Matangazo ya kibiashara

Eugène Nkuranyabahizi, ambaye ni kutoka jamii ya wahutu ana umri wa miaka 41, na anadai kwamba ni raia kutoka Burundi. Alikamatwa may 29 mwaka 2013 nchini Norway, ambako aliishi tangu mwaka 1999.

Rwanda iliomba tangu mwezi agosti mtuhumiwa huyo atumwe nchini humo, ikimtuhumu kuwa na nadharia ya mauwaji ya kimbari na kuhusika katika mauwaji hayo yaliyotokea mwaka 1994. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa watu 800.000 kutoka jamii ya watutsi na wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa katika kipindi kisiyozidi miezi mitatu.

Eugène Nkuranyabahizi, anatuhumiwa kuhusika katika mauwaji yaliyotokea katika vijiji vya Nkakwa na Cyahinda, ambako watu 7.500 waliuawa aprili mwaka 1994.

Mshukiwa huyo anakanusha tuhuma dhidi yake, huku akipinga kutumwa Rwanda.

Mahakama ya Stavanger, kusini magharibi mwa Norway, imesema kwamba madai ya mtuhumiwa huenda yana msingi, na kubaini kwamba inaendelea kumshikiliya wakati uchunguzi ukiendelea.

Mahakama imebaini pia kwamba mtuhumiwa huyo atapewa haki zake zote za msingi, na kesi yake itasikilizwa kwa kuheshimu sheria.

Eugène Nkuranyabahizi anaweza akakata rufaa nchini Norway.

Uamzi huo wa kumtuma unakuja siku moja baada ya kuanza maadhimisho ya miaka 20 ya mauwaji ya kimbari yaliyotokea mwaka 1994.

Mwaka uliopita Norway, ilimtuma nchini Rwanda mshukiwa mwengine kutoka Rwanda Charles Bandora, ambaye alihukumiwa kifungo cha maika 21 jela.

Mwaka jana pia alitumwa nchini Rwanda Adi Bugingo, ambaye inasadikiwa kuwa alichangiya katika mauwaji ya maefu ya raia kutoka jamii ya wtutsi.