URUSI-UKRAINE-DIPLOMASIA

Urusi iko tayari kutafutia ufumbuzi mgogoro wa Ukraine

Makabiliano kati ya polisi na wanaharakati wanaounga mkono Urusi mjini Kiev, nchini Ukraine.
Makabiliano kati ya polisi na wanaharakati wanaounga mkono Urusi mjini Kiev, nchini Ukraine. REUTERS/Mikhail Maslovsky

Viongozi wa Umoja wa Ulaya, Urusi, Marekani na Ukraine watakutana juma lijalo kuzugumzia hali ya kiusalama na kisiasa inayoendelea mashariki mwa Ukraine. Baada ya waakazi wa jimbo la Crimea kupiga kura ya maoni ya kuhamia Urusi, wakaazi wa miji ya Mashriki wanaaandamana kutaka kujitenga na Kiev na kujiunga na Moscow.

Matangazo ya kibiashara

Mataifa ya Magharibi yameendelea kuishtumu Urusi kuhusika moja kwa moja na kudora kwa hali ya usalama na siasa nchini Ukraine.

Muungano wa majeshi ya nchi za Magharibi NATO unakutana jijini Paris nchini Ufaransa kujadili hali ya usalama nchini Ukraine na Katibu mkuu wa majeshi hayo Rass Mussen amesema kwamba Urusi haina lingine bali kuondoa majeshi yake nchini Ukraine ili suluhu lipatikane.

Hayo yakijiri, hali ya sintofahamu inaendelea kutanda mjini Kiev, baada ya hio jana wanaharakati wanao unga mkono Urusi na wale wanaounga mkono serikali ya Kiev kuandamana, huku maelfu ya wanajeshi wa Urusi wakiendelea kutumwa kwenye mpaka wake na Ukraine, lakini matumaini ya kidiplomasia yameonekana kufuatia kutangazwa kwa mazungumzo hivi karibuni kuhusu mzozo unaoendelea nchini Ukraine.

Marekani, Urusi, Ukraine na Umoja wa Ulaya watakutana kwa mazungumzo juma lijalo, katika mji wa nchi mojawapo ya Ulaya ambayo haijatajwa, ili kujadili mzozo wa mashariki-magharibi tangu mwishoni mwa vita baridi.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Mareakni, John Kerry, ambaye amekua akiituhumu Urusi kuwa ndio chanzo cha mgogoro wa Ukraine, ambako wanaharakati wanaounga mkono Urusi wamedhibiti tangu jumapili majengo ya serikali katika miji mikubwa mitatu, amependekeza kwamba kuweko na mataifa manne ambayo yatashiriki mazungumzo hayo.

Moscow haijakataa kushiriki katioka mazungumzo hayo, huku ikiomba wanaharakati wanaounga mkono washirikishwe.

Rais wa Urusi, Vladimir Poutine akizungumzia kuhusu mzozo wa Ukraine.
Rais wa Urusi, Vladimir Poutine akizungumzia kuhusu mzozo wa Ukraine. REUTERS/Alexei Druzhinin

Rais wa Ukraine Vladmir Putine amekutana leo asubuhi na serikali yake ili kujadili ushirikiano wa kiuchumi na Ukraine, baada ya uamzi wa kuchunguza bei ya gesi inayoagizwa kwa asilimia 80 mjini Kiev.