UN-ITALIA-Usalama wa chakula

Mkutano wa kimataifa kuhusu chakula unafanyika Roma Italia

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon akifungua mkutano wa kimataifa kuhusu chakula unaofanyika mjini Roma Italia.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon akifungua mkutano wa kimataifa kuhusu chakula unaofanyika mjini Roma Italia. REUTERS/Kacper Pempel

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN, Ban Ki Moon amesema kuwa dunia inaweza kufikia malengo ya kuzuia kukumbwa na baa la njaa iwapo kutakuwa na juhudi za pamoja za kukabiliana na ukame.

Matangazo ya kibiashara

Ban ameyasema hayo wakati wa mkutano wa kimataifa kuhusu chakula unaofanyika mjini Roma Italia, ambapo wataalamu wa masuala ya kilimo na usalama wa chakula wanakutana kujadili namna ya kukabiliana na ukame na kuzuia baa la njaa kuikumba dunia.

Katibu mkuu Ban amesema kuwa lazima juhudi zifanyike sasa akitolea mfano nchini ya Sudan Kusini ambayo alitembelea juma hili na kuongeza kuwa mamilioni ya raia sio kwa nchi hiyo pekee hata dunia kwa ujumla inakabiliwa na ukame iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa.

Kwenye mkutano huo katibu mkuu Ban amewakumbusha viongozi wa dunia kuwa mwaka 2014 ni mwaka wa kilimo kama ulivyotangazwa na Umoja wa Mataifa na kwamba lazima wakulima wadogowadogo wawezeshwe na nchi zao.