MALI-MNLA-Mapigano

Mali: Mazungumzo ya amani yakumbwa na kizungumkuti

Rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keïta.
Rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keïta. AFP PHOTO / STRINGER

Serikali ya Mali imetangaza vita dhidi ya “magaidi”, siku mbili baada ya mapigano makali kutokea katika mji wa Kidal (kaskazini mwa nchi), ambako ni ngome kuu ya waasi kutoka jamii ya Tuareg. Kwa mujibu wa serikali ya Mali, maafisa 30 wa serikali wametekwa nyara na waasi. Kulingana na taarifa za Umoja wa Mataifa, watu wanane wameuawa.

Matangazo ya kibiashara

Makabiliano makali yalitokea kati ya jeshi na makundi ya waasi wakati waziri mkuu wa Mali, Moussa Mara, alikua zirani katika mji wa Kidal kilomita 1,500 kaskazini mashariki na mji wa Bamako.

Katika makabiliano hayo watu 36 waliuawa wakiwemo wanajeshi wanane, na wengine zaidi ya 30 walitekwa nyara, kulingana na taarifa iliyotolewa na waziri wa ulinzi Soumeylou Boubeye Maïga.

Wapiganaji wa kundi la waasi la MNLA kutoka jamii ya Tuareg katika mji wa Kidal.
Wapiganaji wa kundi la waasi la MNLA kutoka jamii ya Tuareg katika mji wa Kidal. REUTERS/Cheick Diouara

Kundi la waasi la MNLA limekiri kwamba zaidi ya wanaheshi kumi wa Mali na wafungwa thelathini waliuawa, na wafungwa wengine wawili walijeruhiwa, na baadaae walikabidhiwa shirika la msalaba mwekundu.

Hapo jana ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Mali Minusma ilifahamisha kwamba raia wawili wa kawaida na maafisa sita wa serikali waliuawa katika mji wa Kidal, bila hata hivo kutoa taarifa zaidi.

Aliporejea mjini Bamako, hapo jana jioni, waziri mkuu wa Mali, Moussa Mara amefahamisha kwamba serikali inafanya kila lilio chini ya uwezo wake kuhakikisha kwamba watu waliotekwa nyara na waasi wanaachiliwa.

Kuotokana na machafuko hayo,” magaidi wametangaza vita nchini Mali, kwa hio Mali imo katika vita dhidi ya magaodi, amesema waziri mkuu huyo wa Mali katika hatua ya mwisho ya ziara yake katika mji wa Gao kaskazini mwa Mali.

Wakati huo huo serikali ya Marekani imetoa wito wa kuzuia machafuko na kuachiwa huru kwa mateka thelathini walitekwa nyara.

Kauli hiyo imetolewa na msemaji wa wizara ya mambo ya Nje wa Marekani Jen Psaki katika taarifa yake kwa vyombo vya habari na kuomba pande zote kuachana na vurugu na vitendo vyovyote vinavyoweza kuhatarisha maisha ya wananchi

Rais wa zamani wa Burundi, Pierre Buyoya akiwa kwa sasa muakilishi wa Umoja wa Afrika nchini Mali.
Rais wa zamani wa Burundi, Pierre Buyoya akiwa kwa sasa muakilishi wa Umoja wa Afrika nchini Mali. © Elyse Ngabire, journaliste à l’hebdomadaire Iwacu

Kauli kama hiyo imetolewa na wawakilishi wa jumuiya ya kimataifa akiwemo Pierre Buyoya ambaye ni mwakilishi mkuu wa Umoja wa Afrika kwa Ukanda wa Sahel.

“Tunalaani kwa nguvu zote utekaji nyara huo wa wafanyakazi, tunalaani udhibiti usio halali wa ofisi ya mkuu wa mkoa na wa majengo ya serikali uliofanyika na makundi ya wanamgambo. Hatuelewi ni kwa nini ziara ya waziri mkuu katika eneo hilo inaweza kusababisha vitendo kama hivyo”, amesema Buyoya.

Machafuko haya yamezua hisia mbalimbali na kukituhumu kikosi cha Ufaransa kilioko Mali “Force Serval” na ofisi ya Umoja wa Mataifa pamoja wa Ufaransa kwa kuwaunga mkono waasi wa MNLA.

Wanajeshi wa Mali katika mji wa Kidal wakikabiliana na makundi ya waasi.
Wanajeshi wa Mali katika mji wa Kidal wakikabiliana na makundi ya waasi. REUTERS/Joe Penney

Jeshi la Mali limefahamisha kwamba limepeleka wanajeshi wa ziada ili kakabiliana na makundi ya waasi ili kujaribu kureh=jesha mji wa kidali kwenye himaya yake.