Jeshi la Pakistani lazima shambulio la Taliban mjini Karachi
Imechapishwa: Imehaririwa:
Viongozi nchini Pakistan wametangaza wamefaanikiwa kuzima shambulio kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa mjini Karachi nchini Pakistan baada kundi la wanamgambo wa Taliban kushambulia kwa muda wa saa kumi na mbili na kusababisha vifo vya watu 28 wakiwemo waasi 10. Shambulio hilo la wanambgambo wa Taliban ni ishara tosha ya udhaifu wa vikosi vya usalama katika kulinda vituo muhimu husasan ambavyo vinatakiwa kuwa na ulinzi mkali.
Shambulio hilo kubwa kuwahi kushuhudiwa katika mji huo wa kiuchumi nchini Pakistan, umesababisha shuhguli zote za usafiri wa ndege kupwaya kuanzia jana Jumapili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jinnah.
Hata hivyo shughuli hizo zinataraji kuanza tena baade jioni hii kulingana na msemaji wa mamlaka ya shughuli za usafiri wa angani Abid Ali Khan.
Kundi la Taliban kutoka Pakistan la TTP limefanya shambulio ambalo lilianza tangu saa kumi na mbili jioni saa za kimataifa na kusitishwa saa kumi na mbili baadae pale kikosi maalum cha jeshi kuingilia kati na kuwauawa wapiganaji 10 wa Taliban.
Akizungumza na vyombo vya habari, msemaji wa jeshiSibtain Rizvi amesema wamezima shambulio na wamefaanikiwa kuwauawa washambuliaji wote walioendesha shambulo hilo.
Shambulio hilo limegharimu maisha ya watu 28 wakiwemo waasi 10, na wafanyakazi wa uwanja wa ndege.
Kundi la TTP linaendesha mashambulizi tangu mwaka 2007 dhidi ya serikali ya Islamabad inayotuhumiwa na kundi hilo kuwa ya kimagharibi.
Akijigamba kundi lake kuhusika na shambulio hilo, msemaji wa kundi hilo Shahidullah Shahid amesema shambulio hilo linalenga kulipiza kisase dhidi ya kifo cha kiongozi wao Hakimullah Mehsud aliye uawa siku za hivi karibuni na shambulio la ndege zisizokuwa na rubani za Marekani.