DRC-Usalama-Siasa-Sheria-Haki za binadamu

Kesi ya mauaji ya Mamadou N'dala inaendelea kusikilizwa

Jaji mkuu wa Korti ya kijeshi katika mkoa wa Kivu Kaskazini, Kanali Joseph Maya Makako (katikati) Oktoba 1, wakati wa ufunguzi wa kesi ya mauaji ya Mamadou N'dala.
Jaji mkuu wa Korti ya kijeshi katika mkoa wa Kivu Kaskazini, Kanali Joseph Maya Makako (katikati) Oktoba 1, wakati wa ufunguzi wa kesi ya mauaji ya Mamadou N'dala. AFP PHOTO / ALBERT KAMBALE

Kanali mamadou N'dala Moustafa, afisaa maarufu wa jeshi la Congo (FARDC), akiwa pia shujaa wa ukombozi wa Goma, aliuawa Januari 2 kwa roketi karibu na mji wa Beni, Kivu Kaskazini. Hadi leo hajafahamika aliye tekeleza na kuhusika na kifo chake.

Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya washtakiwa ishirini wameanza kusikilizwa, ambapo baadhi ya watuhumiwa watasikilizwa jumatatu wiki hii

Katika wiki ya kwanza, kesi ya kifo cha Sajenti Ndongala, aliye kuwa dereva wa N'dala, ambaye pia anashukiwa kuhusika na kifo cha afisa huyo ilisikilizwa kwa muda mrefu.

Mashahidi wapya na watuhumiwa wanatazamiwa kusikilizwa wiki hii. Raia, wafanyakazi wa serikali pamoja na wanajeshi akiwemo afisaa anaye tuhumiwa kula njama za kumuua N'dala watasikilizwa..

Mashirika ya kiraia kaskazini mwa mkoa wa Kivu Kaskazini yamebaini kwamba yataendelea kuomba wasikilizwe mashahidi watatu waliyofikishwa mbele ya tume iliyoendesha uchunguzi wa kifo cha Mamadou N'dala, ikiwa ni pamoja na dereva wa taxi aliyeshuhudia shambulio dhidi ya gari aliyokuwemo N'dala na watu wengine watu wali ambao hawakutajwa. Mashirika hayo ya kiraia yameomba kufanyike uchunguzi wa kina kuhusu kifo cha Ndongala, ambaye mashirika hayo yanadai kwamba aliuawa katika mazingira ya kutatanisha.

Hata hivo Waziri wa habari akiwa pia msemaji wa serikali, Lambert Mende, amesema hakuhitajiki uchunguzio wowote, kwani Ndongala, alifariki kutokana na ugonjwa wa kawaida.