Brazil-Uchaguzi-Siasa

Brazil: Marina Silva aamua kupambana katika duru ya pili

Siku moja baada ya duru ya kwanza ya uchaguzi, Marina Sila mwanamaziongira, ambaye alishindwa katika duru ya kwanza, awatolea wito wagombea waliofaulu katika duru yakwanza.
Siku moja baada ya duru ya kwanza ya uchaguzi, Marina Sila mwanamaziongira, ambaye alishindwa katika duru ya kwanza, awatolea wito wagombea waliofaulu katika duru yakwanza. REUTERS/Nacho Doce

Kampeni za uchaguzi wa urais kwa duru ya pili zimeanza nchini Brazil, baada ya kutopatikana mshindi katika duru ya kwanza ya uchaguzi, huku rais anaye maliza muda wake, Dilma Rousseff akiongoza kwa asilimia zaidi ya 40 ya kura.

Matangazo ya kibiashara

Marina Silva, ambaye ni mwanamazingira alipata asilimia ndogo ya kura na kuchukua nafasi ya tatu baada ya Aecio Neves.

Hata hivo marina Silva ameamua kuingia katika duru ya pili ya uchaguzi, akibaini kwamba ana imani kwamba atashinda uchaguzi huo.

Hayo yakijiri, mwanamazingira huyo anatazamiwa kukutana Jumatano wiki hii na washirika wake wa karibu kutoka vyama vya kisoshalisti, ili kuamua iwapo ataanzisha kampeni ya kugombea kiti cha rais katika duru ya pili ya uchaguzi.

Wakati huo huo rais wa Brazil Dilma Roussef kutoka mrengo wa Kushoto na mpinzani wake Aecio Neves wa chama cha Social Demokrate, wameanza mchakato wa kutafuta kura za mshindi wa tatu katika duru ya kwanza ya uchaguzi Marina Silva.

Duru ya pili imepangwa kufanyika Octoba 26 mwaka huu ambapo rais Dilma Roussef aliibuka mshindi katika duru ya kwanza kwa kujipatia asilimia 41.5.

Mpinzani wake Aecio Neves alijizolea asilimia 33.5 ya kura na sasa ameanza harakati za kuwashawishi wafuasi wa mrengo wa kushoto waliokata tamaa na kumpigia kura Marina Silava ambaye aalipata asilimia 21.3 ya kura.