EU-ISIL

EU: Jihadi kitisho kwa bara la Ulaya

Capture d'écran d'une vidéo de propagande.
Capture d'écran d'une vidéo de propagande. AFP PHOTO / YOUTUBE

Mawaziri wa mambo ya ndani kutoka mataifa ya Ulaya wanakutana leo alhamisi mjini Luxembourg kujadili uwezekano wa kuzuia raia wa mataifa hayo wanaosafiri kujiunga na makundi ya wapiganaji wa kiislam.

Matangazo ya kibiashara

Kujiunga kwa raia hao katika makundi ya kijihadi imekua ni tishio kwa mataifa ya Ulaya na marekani, ambayo baadhi ya raia wao wamejiunga na wapiganaji wa dola la Kiislam, nchini Syria na Iraq.

Mawaziri hao wa mambo ya ndani kutoka mataifa 28 wanachama wa Umoja wa Ulaya wanatazamia kukutana kwa mara ya kwanza jumatano wiki hii katika mji wa
Luxembourg na wawakilishi wa mitandao ya kijamii, Google, Youtube, Facebook na Twitter, kwani raia hao wanaosafiri kujiunga na makundi hayo ya kiislam wamekua wakipata hamasa kupitia mitandao hiyo ya kijamii.

Hata hivo mataifa ya magharibi yanaendesha vita kwa njia moja ama nyingine, hususan kuisaidia kijeshi seriklai ya Iraq, kuwasaidia waasi wa Syria na kubana kiuchumi kundi hilo la Dola Kiislam ili kuhakikisha kuwa limesambaratishwa kabisa.