UTURUKI-SYRIA-IRAQ-IS-Marekani-Mapigano-Usalama

Uturuki haijaafikiana mkataba mpya na Marekani

Ahmet Davutoglu, waziri mkuu wa Uturuki.
Ahmet Davutoglu, waziri mkuu wa Uturuki. REUTERS/Stringer

Uturuki imebaini kwamba hakuna makubaliano mapya kati yake na Marekani unaoruhusu Marekani na washirika wake kutumia maeneo yake kwa kuweza kuendesha mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislamu nchini Iraq na Syria.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa chanzo cha serikali, hakuna mkataba wowote na Washington kuhusu utumiaji wa maeneo ya kijeshi ya Uturuki kwa muungano unaoendesha mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam, lakini mazungumzo kuhusu suala hilo yameanzishwa, chanzo kiliyo karibu na Waziri mkuu wa Uturuki, Ahmet Davutoglu, kimeiyambia Reuters.

“ Msimamo wetu uko wazi, hakuna makubaliano mapya na Marekani”, chanzo cha serikali kimesisitiza, huku akikumbusha kwamba makubaliano yaliopo wakati huu kati ya Uturuki na Marekani yanaruhusu tu jeshi la Marekani kutumia eneo la kijeshi la Incirlik liliyo karibu na mji wa Adana kusini mwa Uturuki kwa shughuli za kiutu au kibinadamu.

Jumapili wiki iliyopita, mshauri wa masuala ya usalama ya kitaifa kwenye Ikulu ya Washington, Susan Rice, amekua amekua amepongeza kuwa majeshi ya muungano yatatumia maeneo ya kijeshi ya Uturuki dhidi ya wapiganji wa Dola la Kiislam.

“ Serikali ya Uturuki imesema kwamba maeneo ya kijeshi yanaweza kutumiwa na majeshi ya muungano, Marekani au wengine kwa kuendesha mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam nchini Syria na Iraq”, amesema Susan Rice kwenye kituo cha televisheni ya Marekani NBC, huku akibaini kwamba ni makubalianao mapya kati ya Uturuki na Marekani.

Susan Rice amebaini pia kwamba serikali ya Uturuki ilikubali kutoa baadhi ya maeneo yake ya kijeshi kwa mafunzo ya kijeshi ya waasi wa Syria wenye msimamo wa wastani.

Kwa sasa Uturuki imekataa kujiunga na muungano wa kijeshi wa kimataifa unaoongozwa na Marekani kwa misingi ya kwamba mashambulizi ya angani dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam yanaweza kuimarisha kambi ya rais wa Syria Bashar al-Assad.