SYRIA-MAREKANI-UTURUKI-ISIL-KOBANE-Usalama

Syria: hali ya usalama bado ni tete Kobane

Mapigano yaendelea kurindima katika mji wa Kobane, nchini Syria.
Mapigano yaendelea kurindima katika mji wa Kobane, nchini Syria. REUTERS/Umit Bektas

Makabiliano makali yanaendelea katika mji wa Kobane katika mpaka wa Uturuki na Syria kati ya wapiganaji wa Dola la Kiislam na wapiganaji wa kikurdi.

Matangazo ya kibiashara

Wapoganaji wa Dola la Kiislam wamekuwa wakikabiliana na wapiganaji wa Kikurdi kwa majuma matatu sasa, huku jeshi la Marekani na Saudi Arabia likiendeleza mashambulizi ya anga dhidi ya kundi hilo.

Uturuki imekubali Marekani kutumia nchi yake kutoa mafunzo ya kijeshi kwa wapiganaji wa Kikurdi na waasi wa Syria wasiokuwa na msimamo mkali kusaidia kukabiliana na wapiganaji hao wa Dola la Kiislam.

Wakimbizi wa Kobane wakiwa katika kambi ya wakimbizi iliyo karibu na mji wa Suruc, Oktoba 11 mwaka 2014.
Wakimbizi wa Kobane wakiwa katika kambi ya wakimbizi iliyo karibu na mji wa Suruc, Oktoba 11 mwaka 2014. REUTERS/Umit Bektas

Marekani imesema mapigano yanayoendelea katika mji wa Kobane, hayatabadilisha mpango wake wa kulidhohofisha kundi hilo nchini Syria na Iraq.
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa ikiwa, juhudi za haraka hazitannyika kuudhibiti mji huo ambao asilimia 40 upo mikononi mwa Islamic State, maafa na uharibu huenda yakashuhudiwa.

Maandamano ya kupinga kudhibitiwa kwa mji wa Kobane na wapiganaji wa ISOktoba 11 mwaka 2014.
Maandamano ya kupinga kudhibitiwa kwa mji wa Kobane na wapiganaji wa ISOktoba 11 mwaka 2014. REUTERS/Gonzalo Fuentes

Wakati mapigano hayo yakiendelea, wakuu wa majeshi kutoka nchi zinazoshiriki katika mashambulizi ya anga dhidi ya wapiganaji wa dola la Kiislam wanakutana leo Jumanne jijini Washingtoin DC, nchini Marekani kuthathmini maendeleo ya mashambulizi hayo.