Pata taarifa kuu
CHINA-HONG KONG-Maandamano-Siasa

Hong Kong: Askari polisi wafutwa kazi kwa kukiuka sheria

Mbunge kutoka chama cha upinzani kinachounga mkono utawala wenye misingi ya kidemokrasia Hong Kong, apigwa na polisi.
Mbunge kutoka chama cha upinzani kinachounga mkono utawala wenye misingi ya kidemokrasia Hong Kong, apigwa na polisi. Philippe Lopez / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Baada ya polisi kufaulu kuondoa vizuizi kwenye barabara Jumatau na Jumanne wiki hii, makabiliano kati ya waandamanaji na polisi yameendelea kushuhudiwa usiku wa kuamkia leo Jumatatu mjini Hong Kong.

Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji wamekua wapeiga kambi mbele ya jengo la serikali mjini Hong Kong, wakimtaka Waziri mkuu wa serikali katika jimbo la Hong Kong ajiuzulu. Wakati huohuo polisi imewakamata waandamanaji wengi mapema leo jumatatu asubuhi.

Hali hii ya makabiliano kati ya waandamanaji na polisi huenda ikazua hali ya machafuko katika mji wa Hong Kong.

Hata hivo polisi imekua ikijaribu kutumia nguvu ili kuwaondoa waandamanaji katika maeneo wanayo kaliwa, hususan barabara zinazoingia kwenye jengo la serikali ambapo kuna ofisi ya Waziri mkuu.

Baadhi ya waandamanaji wamekua wakifanyiwa vitendo vya unyanyasaji na askari polisi. Mwanasiasa mmoja wa upinzani alifanyiwa kipigo na polisi Jumanne wiki hii, ambapo baadhi ya askari poli walimdhalilisha mbele ya watu. Tukio hilo lilirushwa kwenye televisheni ya taifa.

Mapema Jumatatau asubuhi wiki hii polisi imelani kitendo hicho na kubaini kwamba askari polisi waliohusika waliadhibiwa kwa mujibu wa sheria.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.