NIGERIA-BOKO HARAM-Usalama

Nigeria: Boko Haram yatiliana mkataba na serikali

Wazazi wa wanafunzi wasichana waliotekwa nyara Aprili 14 mwaka 2014 na  Boko Haram, wakiwa katika mkutano na mkuu wa mkoa wa BornoBorno, Aprili 22 mswaka 2014.
Wazazi wa wanafunzi wasichana waliotekwa nyara Aprili 14 mwaka 2014 na Boko Haram, wakiwa katika mkutano na mkuu wa mkoa wa BornoBorno, Aprili 22 mswaka 2014. REUTERS/Stringer

Viongozi wa Nigeria wametangaza Ijumaa Oktoba 17 kwamba wamefikia makubaliano ya kusitisha mapigano na wapiganaji wa kiislam wa kundi la Boko Haram.

Matangazo ya kibiashara

Makubaliano mengine ambayo pande hizo mbili zimeafikiana ni kuwachilia huru wanafunzi wasichana 200 waliotekwa nyara miezi sita iliyopita katika mji wa Chibok, akaskazini mashariki mwa Nigeria. Tukio hilo lilizua hasira duniani.

“ Makubaliano yameafikiwa kati ya serikali ya Nigeria na kundi la Jama'atu Ahlis Sunna Lidda'awati wal-Jihad”. amesema mkuu wa majeshi ya Nigeria, Alex Badeh.

“ Nimetoa amri kwa viongozi mbalimbali wa kijeshi kuheshimu makubaliano hayo haraka iwezekanavyo”, ameongeza Badeh.

Katika mahojiano na AFP, ikulu ya Nigeria imetangaza kwamba imeafikiana kusitisha mapigano na na kundi la Jama'atu Ahlis Sunna Lidda'awati wal-Jihad, ambalo linalojulikana zaidi kwa jina la Boko Haram.

Wapiganaji hao wa Kiislam wamekua wakiendesha harakati zao katika ngome yao kaskazini-mashariki mwa Nigeria kwa kipindi cha miezi kuni na nane.

Kiongozi wa kundi la Boko Haram, Abubakar Shekau, akiwa na wapiganaji wake,  Aprili 13 mwaka 2014.
Kiongozi wa kundi la Boko Haram, Abubakar Shekau, akiwa na wapiganaji wake, Aprili 13 mwaka 2014. AFP PHOTO / BOKO HARAM

Kundi hilo likikiri mara kadhaa kuhusika na mashambulizi kadhaa ya mabomu katika mji mkuu wa Abuja, na liliwaua, kulingana na taarifa iliyotolewa na shrika lakimataifa la haki zabinadamu la Human Rights Watch, zaidi ya raia elfu mbili tangu mwanzo wa mwaka.

Hassan Tukur, mshirika wa karibu wa rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, ametangaza pia kwamba seriklai na kundi hilo wameafikiana kuwaachilia huru wanafunzi wasichana 216 ambao bado wanashikiliwa na wanajihadi tangu walipotekwa nyara Aprili 14 mwaka 2014.
 

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, Mei 9 mwaka 2014.
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, Mei 9 mwaka 2014. REUTERS/Afolabi Sotunde/Files

Tangazo hil linatolewa wakati ambapo rais Goodluck Jonathan atatangaza hivi karibuni kugombea kwenye kiti cha urais kwa muhula wa pili. Chaguzi zimepangwa kufanyika mwezi Februari mwakani.