ISRAELI-PALESTINA-IS

Israel yatiwa wasiwasi na raia wake kujiunga na IS

REUTERS/Finbarr O'Reilly

Vyombo vya usalama nchini Israel vimebaini kwamba daktari raia wa Israel mwenye asili ya kiarabu alifariki hivi karibuni nchini Syria, baada ya kujiunga na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam. Hali hii imewatia wasiwasi viongozi wa Israel.

Matangazo ya kibiashara

Daktari huyo ambaye anajukikana kwa jina la Abou al-Qiyan inasadikiwa alifariki mwezi wa Agosti nchini Syria, wakati alipokua katika uwanja wa vita, baada ya kujiunga na kundi la wapiganaji wa Kiislam.

Kijana huyo alikua mkaazi wa kijiji cha Wabeduwi kusini mwa Israel, alikua daktari, na alisomea Jordan kabla ya kuajiriwa kwenye hospital ya Israel. Inaaminika kuwa kijana huyo alikua alipata elimu ya kutosha katika taaluma yake ya udaktari kulingana na vyanzo vya hospitali iliyomuajiri.

Othmane Abou al-Qiyan, alikosekana tangu mwezi wa Juni mwaka 2014. Kaka yake alikamatwa na kutuhumiwa kumsadia nduguye kwa kujiunga na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam nchini Syria.

Kwa mujibu wa vyombo vya usalama nchini Israel, zaidi ya Waisrael wenye asili ya kiarabu walijiunga na wapiganaji wa Dola la Kiislam, wachache baadhi yao ndio walisajiliwa katika kundi hilo.

Viongozi wa Israel wana hofu kwamba huenda watu hao wakarejea nchini Israel na kuanza kutekeleza mashambulixzi mbalimbali ya kujitoa mhanga.