MALI-Uchumi-Ulinzi

Mali: Boubeye Maiga anyooshewa kidole kwa kashfa ya ufisadi

Soumeylou Boubèye Maïga.
Soumeylou Boubèye Maïga. AFP/Georges Gobet

Waziri wa zamani wa ulinzi wa Mali, Soumeylou Boubeye Maiga amemjibu kwenye kurasa 22 Mkaguzi mkuu wa serikali, ambaye anaongoza tume inayochunguza ufisadi wa mali ya umma nchini Mali.

Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti ya muda, Mkaguzi mkuu wa serikali amenyooshea kidole kasoro zilijitokeza katika soko za uzabuni, hasa wakati wa kununua vifaa vya kijeshi.

Waziri wa zamani wa ulinzi, Soumeylou Boubeye Maiga, amepinga uamuzi wa wa Mkaguzi mkuu wa serikali wa kuendesha uchunguzi kuhusu ununuzi wa vifaa vya jeshi.

"Mkaguzi hana mamlaka juu ya sheria zetu, kwa kukamilisha kazi yake na kutekeleza aliyoombwa. Watu wengi wanataka wachukuliwe kama watakatifu ambao hawana doa la kashfa yoyote”, amesema Maiga.

Kwa kujizuia kutaja hadharani mambo ya usalama wa taifa, Soumeylou Boubeye Maiga, Waziri wakati huo, amedai katika kitabu cha kurasa ishirini na mbili alichoandika, kwamba hawezi kutoa siri ya jeshi.

"Mpaka sasa sijaona serikali ambayo inaweka hadharani mambo ya kijeshi,"ameongeza Maiga.
"Siri ya ulinzi," neno hili limeshapitwa na wakati. Kulingana na taarifa mbalimbali, silaha zilinunuliwa.

Akijitetea Soumeylou Boubeye Maiga amesema hawezi kusema hadharani mambo ya ya jeshi kwa kuhofia usalama wa taifa, huku akibaini kwamba rais wa taifa ambaye ndiye amiri jeshi alikua akipewa taarifa zote kuhusu ununuzi wa vifaa vya jeshi.