MISRI-Usalama

Misri: shambulio la bomu mbele ya chuo kikuu cha Cairo

Polisi ya Misri ikiwa kwenye eneo kulikotokea shambulio mbele ya chuo kikuu cha Cairo, Oktoba 22 mwaka 2014.
Polisi ya Misri ikiwa kwenye eneo kulikotokea shambulio mbele ya chuo kikuu cha Cairo, Oktoba 22 mwaka 2014. AFP PHOTO / KHALED DESOUKI

Watu zaidi ya kumi wamejeruhiwa leo Jumatano Oktoba 22 katika shambulio la bomu liliyotokea mbele ya chuo kikuu cha mjini Cairo. Askari polisi saba akiwemo afisa wa cheo cha jenerali ni miongoni mwa watu waliyojeruhiwa.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo limetokea mbele ya majengo ya kitivo cha uhandisi katika chuo kikuu cha Cairo. Siku ya Jumanne, mwanafunzi wa kitivo cha uhandisi katika chuo kikuu cha Alexandria alifariki katika hospitali. Mwanafunzi huyo alikua alijeruhiwa hivi karibuni katika makabiliano kati ya waandamanaji na polisi.

Bomu hilo limekua limewalenga maafisa wakuu wa polisi ambao walikua wakipiga doria mbele ya chuo kikuu. Mwaka jana maafisa kadhaa wa polisi waliuawa katika sehemu hiyo kuliko lipuka bomu leo Jumatano. Wakati huo hakuna raia aliye jeruhiwa. Raia wamekua wakipoteza maisha katika mashambulio hayo ambayo yamekua yakivilenga vikosi vya usalama.

Wiki iliyopita watu ishirini walijeruhiwa katika mji wa Cairo na Tanta katika eneo la Delta, kufuatia mashambulizi mbalimbali. Kwa sasa mashambulizi yamekua yakisababisha hasira kwa raia zaidi ya hofu. Hasira dhidi ya wafuasi wa kundi la Brotherhood, ambao wanatuhumiwa kutekeleza mashambulizi hayo, lakini pia hasira dhidi ya uzembe wa serikali katika kukabiliana na ugaidi. Hali ambayo inaweza kusababisha kupitishwa kwa hatua kali za usalama zaidi ya ziliyopo.