UKRAINE-Usalama

Ukraine: Mji wa Donetsk washambuliwa kwa mabomu

Moshi kupanda hewani kutoka eneo la uwanja wa ndege wa Donetsk baada ya mashambulizi ya mabomu, Oktoba 12, 2014.
Moshi kupanda hewani kutoka eneo la uwanja wa ndege wa Donetsk baada ya mashambulizi ya mabomu, Oktoba 12, 2014. REUTERS/Shamil Zhumatov

Milipuko ya makombora imesikika Jumatatu Oktoba 27 katika mji wa Donetsk, ambao ni ngome ya waasi wa Ukraine, siku moja baada ya uchaguzi wa wabunge.

Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya milipuko ya mabomu ishirini aina ya Grad imesikika Jumatatu Oktoba 27 katika mji wa Donetsk, mashariki mwa Ukraine.

Mabomu hayo yamerushwa na waasi wa ukraine kutokea katika kata ya Poutilovski, yakielekezwa kwenye ngome za jeshi la Ukraine, ambalo bado linashikilia sehemu ya Uwanja wa Donetsk. Ngome ya jeshi la Ukraine katika eneo la Avdiivka imeshambuliwa .

Waasi kwa wao wamebaini kwamba wamezuia mashambulizi yaliyokua yakiendeshwa na jeshi la Ukraine katika mji wa Donetsk. Mashambulizi hayo yanatokea baada ya siku mbili ya hali ya utulivu kuripotiwa.

Mashambulizi hayo yanatokea pia siku moja baada ya uchaguzi wa wabunge uliyofanyika katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali ya Kiev.

Mei 26 siku moja baada ya uchaguzi wa rais, waasi wa Ukraine waliuteka uwanja wa ndege wa Donetsk kabla ya kutimuliwa na jeshi saa chache baadae.

Tangu siku kadhaa zilizopita raia wa mji wa Donbass walikua na wasi wasi kwa kutokea upya kwa mapigano.