FIFA-Soka-michezo

wachezaji 23 wawania tuzo la mpira wa dhahabu 2014

Yaya Touré, mchezaji nyota wa Côte d'Ivoire, ambaye ni miongoni mwa wachezaji 23 waliyoteuliwa na Fifa kwa kuwania tuzo la mpira wa dhahabu 2014..
Yaya Touré, mchezaji nyota wa Côte d'Ivoire, ambaye ni miongoni mwa wachezaji 23 waliyoteuliwa na Fifa kwa kuwania tuzo la mpira wa dhahabu 2014.. REUTERS/Eddie Keogh

Shrikisho la Soka Duniani Fifa limeweka wazi Jumanne Oktoba 28 orodha ya wachezaji watakawania tuzo la mpira wa dhahabu mwaka 2014.

Matangazo ya kibiashara

Fifa imewateua wachezaji 23 kutoka vilabu mbalimbali duniani ambao watawania tuzo hilo.

Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Neymar, Zlatan Ibrahimovic na Arjen Robben ni miongoni mwa wachezaji nyota watakaowania tuzo hilo.
Wachezaji kutoka ujerumani wanaongoza kwa idadi kubwa katika orodha hiyo ya mabingwa wa dunia 23.

Ufaransa imewakilishwa na wachezaji wawili pekee, ambao ni Karim Benzema na Paul Pogba. Franck Ribéry, aliye teuliwa mwaka 2013 hakujikuta katika orodha ya wachezaji nyota watakaowania tuzo hilo ya mpira wa dhahabu.

Yaya Touré balozi pekee wa Afrika katika kinyang'aniro

Yaya Touré ambaye ni mmoja pekee aliye teuliwa kutoka barani Afrika, atawania tuzo hili kwa miaka mitatu mfululizo.

Wachezaji bingwa kutoka barani Afrika ambao ni Didier Drogba, Samuel Eto'o na Asamoah Gyan waliteuliwa miaka iliyopita, na mwaka 2014 hawakujikuta katika orodha.

Ujerumani imewakilishwa na wachezaji sita ambao ni mabingwa wa dunia.

Mwaka 2013, Yaya Touré alijikuta akichukua nafasi ya 12. Mchezaji huyo nyota wa Côte d'Ivoire ameteuliwa kwenye orodha ya wachezaji bingwa wataowania tuzo la mpira wa dhahabu kufuatia ushindi wa klabu yake ya Manchester City katika michuano ya ligi kuu, lakini pia umaarufu wake katika michuano ya ligi yamempa mafanikio makubwa msimu huu.

Wachezaji watatu watapunguzwa kwenye orodha hiyo. Waandishi wa habari, makocha pamoja na manahodha wa timu za taifa watamchagua mmoja kati ya wachezaji hao, ambaye ndiye atakaye pewa tuzo la mpira wa dhahabu, ambayo itatolewa Januari mwaka 2015 katika mji wa Zurich.

Orodha ya wachezaji 23 nyota walioteuliwa kuwania tuzo la mpira wa dhahabu:

Gareth Bale (Wales), Karim Benzema (Ufaransa), Diego Costa (Uhispania), Thibaut Courtois (Ubelgiji), Cristiano Ronaldo (Ureno), Angel Di Maria (Argentina), Mario Goetze (Ujerumani), Eden Hazard (Ubelgiji), Zlatan Ibrahimovic (Sweden), Andres Iniesta (Uhispania), Toni Kroos (Ujerumani), Philipp Lahm (Ujerumani), Javier Mascherano (Argentina), Lionel Messi (Argentina), Thomas Müller (Ujerumani), Manuel Neuer (Ujerumani), Neymar (Brazil), Paul Pogba (Ufaransa), Sergio Ramos (Uhispania), Arjen Robben (Uholanzi), James Rodriguez (Colombia), Bastian Schweinsteiger (Ujerumani), Yaya Toure (Côte d'Ivoire).