ISRAELI-PALESTINA-Siasa-Usalama

Israel: hofu ya “kulipuka” kwa machafuko Jerusalem

Hali ya taharuki yaendelea kutanda Jerusalem, baada ya Israel kutangaza kuendelea na mpango wa ujenzi wa nyumba 1000 katika maeneo mawili mashariki mwa Jerusalem.
Hali ya taharuki yaendelea kutanda Jerusalem, baada ya Israel kutangaza kuendelea na mpango wa ujenzi wa nyumba 1000 katika maeneo mawili mashariki mwa Jerusalem. REUTERS/Ronen Zvulun

Hali ya taharuki imeendelea kutanda katika mji wa Jerusalem baada ya serikali ya Israel kutangaza Jumatatu Oktoba 27, kwamba itaendelea na mpango wake wa ujenzi wa nyumba mpya mashariki ya mji huo.

Matangazo ya kibiashara

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakutana kwa dharura Jumatano oktoba 29 kujadili suala hilo kwa ombi la Jordan.

Uamuzi wa Israel ulishutumiwa na Marekani, Umoja wa Ulaya na nchi kadhaa za Kiarabu, wakati ambapo waziri mkuu wa Israel, Binjamin Netanyahu amejitetea kuhusu ujenji huo. Balozi wa Palestina kwenye Umoja wa Mataifa ameandika barua akiomba taasisi hiyo ya kimataifa kukemea kile alichokiita "uchokozi wa Israel na muendelezo wa Ukoloni katika mji wa Jerusalem ya Mashariki". Riyad Mansour ameiomba jumuiya ya kimataifa kulani kwa pamoja kauli za hivi karibuni za viongozi wa Israel.

Kiongozi mwandamizi wa Fatah chama cha rais Mahmoud Abbas, amesema anatiwa hofu ya kutokea kwa "mlipuko" katika mji mtakatifu iwapo ukoloni utaendelea kwa kasi hiyo. Mapigano kati ya Wapalestina na vikosi vya usalama vya Israel yanaendelea kushuhudiwa kila kukicha. Waandamanaji wamekemea vikwazo viliyowekwa katika misikiti. Ziara ya mkuu wa manispa ya jiji la Jerusalem katika eneo takatifu kwa Waislam Jumanne asubuhi Oktoba 28, imezua hofu ya kuanganishwa mji huo kwa Israel.

Kwa miaka kadhaa, baadhi ya Wayahaudi wenye msimamo mkali wa kidini walidai haki ya kuabudu katika eneo hilo takatifu. Akilaani mipango ya Israel, Nabil Abu Rudeina, msemaji wa rais wa Palestina, amepinga mashambulizi yanayoendeshwa kila siku na Israel dhidi ya wakaazi wa Kiarabu wa mji huo wa Jerusalem. Kwa mujibu wa Rudeina, sera za Israel ni "uchafu hatari usiyokubalika".