Raia wa Mali wafukuzwa Equatorial Guinea
Imechapishwa:
Zaidi ya raia wa Mali, waliofukuzwa nchini Equatorial Guinea, wamewasili katika hali huzuni Jumatatu katika mji mkuu wa Mali, Bamako.
Viongozi wa Equatorial Guinea waliwachukulia watu hao kama wahamiaji haramu. Lakini raia hao wamebaini kwamba si wahamiaji haramu, kwani walikua na vyeti vya kuishi nchini Equatorial Guinea. Watoto wadogo ni miongoni mwa raia hao wa Mali waliofurushwa nchini Equatorial Guinea.
Raia hao wamelaumu vikosi vya usalama vya Equatorial Guinea kwa kuwatendea ukatili wakati walipokua wakikamatwa na kupelekwa jela.
Kwa mujibu wa mashahidi, hali hiyo ilianza kwa kukamatwa kwa raia wengi kutoka Mali katika miji ya Malabo na Bata.
Baadhi raia hao wa Mali wamethibitisha kwamba waliacha mali zao nchi Equatorial Guinea, huku wengine wakibaini kwamba waliacha wanawake na watoto.
Mashahidi wamesema kwamba raia hao wa Mali walifungwa jela kabla ya kusafirishwa hadi nchini mwao.