MFUMO WA JUA-SAYANSI

Mfumo wetu wa jua kuwa na sayari ya tisa, kulingana na watafiti

Kunaweza kuwa na sayari ya tisa katika mfumo wa jua, wamebaini watafiti katika makala iliyochapishwa katika jarida la sayansi za anga la Marekani. Ikiwa na ukubwa zaidi ya mara 10 kuliko dunia, sayari hii inasadikiwa kuwa iko kwenye umbali wa kilomita bilioni 30 kutoka dunia hii kunakoishi viumbe mbalimbali.

Mtazamo wa msanii kuhusu jinsi inaweza kuwa sayari ya tisa ya mfumo wetu wajua.
Mtazamo wa msanii kuhusu jinsi inaweza kuwa sayari ya tisa ya mfumo wetu wajua. REUTERS/R. Hurt/Caltech/IPAC/Handout via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Lakini iko mbali unapoiangalia moja kwa moja. Ni kupitia mlango wa nyuma ambapo wanasayansi wameweza kupata sayari hiyo. Lakini itabidi kutafuta njia ya kuiangalia moja kwa moja ili kupata mzizi wake.

Mfumo wa jua umekua na sayari ya tisa. Dhana hii sio mpya. Imekuwa ni karne moja kukizungumziwa sayari hii, hasa wafuasi wa nadharia ya njama, wanaoiita kwa jina la sayari X. Sayari ambayo ni darubini ya dunia hii ambayo wanasayansi wanaituficha kwa sababu huenda inaundwa na almasi.

Huenda sayari hii hii haipo. Hata hivyo, inawezakana pia kuwa kuna sayari sahihi ya tisa, ambayo inaonekana kuliko hiyo. Ikiwa na ukubwa wa zaidi ya mara kumi kuliko dunia hii, na huenda inapatikana mbali zaidi na mhimili wa Neptune, katika mpaka wa eneo liitwalo Kuiper Belt, kilomita bilioni 30 kutoka dunia hii wanakoishi viumbe mbalimbali. Lakini kwa bahati mbaya iko mbali zaidi unapoichunguza moja kwa moja.

Baada ya kufanya mahesabu, watafiti wana uhakika kwamba dhana hii ni sahihi. Lakini kabla ya kupasisha dhana hii, na kufikiria jina ambalo wanaweza kuita sayari hii mpya. Uchunguzi pekee wa moja kwa moja unaweza kuthibitisha kuwepo sayari hii. Na hii inaweza kuchukua miaka kadhaa.

Mhadhiri na falaki Mike Brown akitoa matokeo ya utafiti wa kisayansi akisema kuwepo kwa sayari ya tisa katika mfumo wetu wa jua.
Mhadhiri na falaki Mike Brown akitoa matokeo ya utafiti wa kisayansi akisema kuwepo kwa sayari ya tisa katika mfumo wetu wa jua. REUTERS/Mario Anzuoni