Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-TALIBAN-USALAMA

Watu wengi wauawa katika shambulio la kujitoa mhanga Kabul

Eneo la shambulio, Machi 29, 2016 Kabul.
Eneo la shambulio, Machi 29, 2016 Kabul. AFP
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Watu wengi wameuawa mapema Jumanne hii asubuhi mjini Kabul katika shambulio la kujitoa mhanga lililotekelezwa na wapiganai wa kundi la Taliban dhidi ya majengo ya serikali yalio karibu na makao makuu ya Idara ya Ujasusi nchi Afghanistan.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani anasema kuwa watu wengi wameuawa ana wengine kujeruhiwa kufuatia shambulizi la kujitoa mhanga wakati wa shughuli nyingi kwenye mji mkuu wa Afghanistan Kabul.

"Rais analaani kwa kauli kali shambulio la kigaidi la asubuhi hii ambalo limesababisha vifo vya watu wengi na watu wengi waliojeruhiwa miongoni mwa raia wenzutu," kwa ujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya rais.

Kundi la wapiganaji wa Taliban limetangaza kuendesha shambulio hilo. Hivi karibuni kundi la wapiganaji wa Taliban lilitangaza kuwa mbioni kuanzisha mashambulizi katika nchi nzima ya Afghanistan.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.