EU-UTURUKI-WAHAMIAJI

EU yatoa msamaha wa viza kwa raia wa Uturuki

Tume ya Ulaya, Bruxelles.
Tume ya Ulaya, Bruxelles. REUTERS/Vincent Kessler

Tume ya Ulaya Jumatano imeziomba serikali za nchi wanachama Umoja wa Ulaya kuchukua hatua za msamaha wa viza kwa raia wa Uturuki wanaotaka kuingia Ulaya kwa malipo ya mkataba ambapo Ankara imeahidi kupunguza wimbi la wahamiaji na wakimbizi barani Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa Tume ni "hatua kubwa" katika suala la viza kwa raia wa Uturuki na ni "ukurasa mpya katika uhusiano wetu na Umoja wa Ulaya," waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu, amepongeza uamuzi huo.

Brussels imepiga kura Jumatano hii katika neema ya msamaha wa viza, kwa raia wa Uturuki wanaosafiri Ulaya, ambapo Ankara imekua ikitoa sharti kwa kuendelea kutekeleza mkataba wake uhusuo uhamiaji pamoja na Umoja wa Ulaya lakini unaoziweka nchi za Ulaya katika matatizo.

Hivi karibuni Uturuki ilitoa shinikizo juu ya suala hili, na kutishia kuhatarisha mkataba wake wa Machi 18 pamoja na Umoja, ambao unaeleza kuwarejesha nchini Uturuki wahamiaji wapya wanaowasili katika visiwa vya Ugiriki, ikiwa ni pamoja na wanaotafuta hifadhi.

Pamoja na kufungwa kwa barabara ya nchi za Balkan, mkataba umepungua kwa kiasi kikubwa shinikizo kwa Umoja wa Ulaya, kwa kupunguza idadi ya wahamiaji kuwasili kila siku katika visiwa vya Ugiriki kutoka pwani ya Uturuki.

Hivyo hofu imeenea katika Umoja wa Ulaya kwamba Brussels inatakiwa kupunguza vikwazo dhidi ya Uturuki, ambayo inashtumiwa kutoheshimu uhuru wa kujieleza na wakati ambapo shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International linaishtumu kuwarejesha makwao kwa nguvu raia wa Syria, ambayo inakumbwa na vita tangu mwaka 2011.

Rais wa Tume ya Ulaya, Jean-Claude Juncker, na Waziri Mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu, "kukaribishwa kushuka kwa idadi ya wahamiaji wanaovuka Bahari ya Aegean", wakati wa mazungumzo ya simu Jumanne hii, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la ANATOLIA, na kuongeza kwamba "walijadili" swala la viza.

Jumatano hii Tume ya Umoja wa Ulaya imewasilisha muswada wa kuiweka Uturuki kwenye orodha ya nchi zilizopewa msamaha wa viza" kwa muda mfupi (siku 90) katika nchi za ukanda wa Schengen, kwa mfumo wa familia, safari za kibiashara au utalii.