Real Madrid yaikatisha tamaa Man City
Imechapishwa: Imehaririwa:
Real Madrid, mabingwa mara 10 wa michuano ya klabu bingwa barani Ulaya (UEFA), wakiwa nyumbani wamefaulu kuwalaza Manchester City kwa bao 1-0, katika mechi iliyopigwa Jumatano hii usiku.
Manchester City walikua wanahitaji bao moja tu la ugenini ili kuingia fainali, lakini hawakubahatika licha ya mkwaju mkali wa Sergio Aguero ulipogonga nyavu za juu za lango la Madrid.
Itafahamika kwamba katika mechi ya awali timu hizi zilitoka sare ya kutofungana, wakati ambapo Manchester City ilikua ikichezea nyumbani.
Bao la vijana wa Zinedine Zidane lilifungwa na Gareth Bale baada ya mchezaji wa Man CityFernando kushindwa kuudhibiti mpira uliopigwa na kiungo huyo hatari wa Real Madrid.
Mashabiki 4,500 wa Man city waliweza kuhudhuria mechi hiyo ugenini, huku wakiwa na matumaini ya timu yao kufanya vizuri.
Manchester City wameondolewa, na sasa Real Madrid wanajiandaa kumenyana na Atletico katika uwanja wa San Siro Mei 28.