DRC-UN-USHIRIKIANO

Serikali DRC yakanusha ripoti ya UN

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila Oktoba mwaka jana katika mji wa Beni.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila Oktoba mwaka jana katika mji wa Beni. © AFP PHOTO/ALAIN WANDIMOYI

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekanusha ripoti ya Umoja wa Mataifa kuwa, jeshi lake na polisi limepewa silaha kutoka Korea Kaskazini, kinyume na sheria za Kimataifa.

Matangazo ya kibiashara

Kinshasa inasema , haijawahi kushirikiana na Pyongyang katika utawala huu wa rais Joseph Kabila.

Watalaam wa Umoja wa Mataifa wanasema, bastola zilizotengenezwa nchini Korea Kaskazini zimekabidhiwa kwa wanajeshi wa serikali na polisi wanaolinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Umoja wa Mataifa imepitisha azimio la kuizuia nchi hiyo kuuza silaha zake kutokana na mradi wake wa Nyuklia.