UTURUKI- JAMII

Mkutano usiyokuwa wa kawaida kufanyika Istanbul

Mkutano na waandishi wa habari kabla ya Mkutano wa kilele Istanbul, Mei 22, 2016.
Mkutano na waandishi wa habari kabla ya Mkutano wa kilele Istanbul, Mei 22, 2016. AFP

Viongozi na mashirika yasiyo ya kiserikali duniani kote wanakutana Jumatatu hii katika mji wa Istanbul kwa ajili ya mkutano usiyokuwa wa kawaida, ili kuboresha uwezo wa kukabiliana na maafa ya kibinadamu yanayosababishwa na migogoro na ongezeko la joto duniani.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu unafadhiliwa na Umoja wa Mataifa.

Pamoja na watu wapatao milioni 60 walioyahaama makazi yao na milioni 125 wanaohitaji msaada duniani, wadau wengi katika suala hili, mataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika mbalimbali wanaamini kwamba mfumo wa sasa wa kibinadamu umefikia katika hali ya kutisha na unahitaji kuhudumiwa.

Lakini karibu watu 6,000 wanaonatarajiwa kushiriki mkutano huo, ikiwa ni pamoja na marais na viongozi wa serikali 60, wanatazamia kujadili namna ya kukabilia na hali hii. Shirika la Madaktari wasio na mipaka (MSF), ambalo linatarajia kusikia "tamko la nia nzuri" wakati ambapo hakuna maendeleo thabiti, limetangaza kwamba halitahudhuria mkutano huo.

Mikutano baina ya nchi mbali ya tukio hili pia inatarajiwa: Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametangaza kuwa atazungumza pamoja na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan Jumatatu hii kuhusu hali ya kidemokrasia nchini Uturuki.

Mkutano huu wa siku mbili ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, unatazamia kuanzisha mfululizo wa "utekelezaji na ahadi thabiti" ili kusaidia nchikujiandaa vizuri kwa kukabiliana na migogoro, kuunda mbinu mpya ya kusimamia ukimbizi na kuhakikisha vyanzo vya kuaminika vya fedha kwa kukabiliana na hali hiyo.

"Hii ni fursa ya kipekee ya kuanzishampango kabambe utakaochukua muda mrefu ili kubadili mfumo uliokuwepo na kukabiliana na mateso wanayoyapata watu wenye maisha duni katika dunia hii," Makamu Katibu Mkuu wa Umoja wa anaye husika na Mambo ya kibinadamu, Stephen O'Brien, ametangaza Jumapili hii.