UFARANSA-GOOGLE

Polisi ya Ufaransa yavamia Ofisi za Google

Kampuni kubwa ya Marekani ya Google Ufaransa inalengwa na uchunguzi wa awali kwa ukwepaji wa kulipa kodi.
Kampuni kubwa ya Marekani ya Google Ufaransa inalengwa na uchunguzi wa awali kwa ukwepaji wa kulipa kodi. Reuters/Jacques Brinon/Pool/File Photo

Msako unaendelea Jumanne hii Mei 24 katika ofisi za kampuni ya Marekani ya Google mjini Paris. Kwa mujibu Ofisi ya mashitaka ya fedha, uchunguzi wa awali ulianzishwa Juni 16, 2015 nchini Ufaransa kwa kosa la ukwepaji wa kulipa kodi na kujitajirisha kinyume cha sheria katika genge la watu walioandaliwa.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa gazeti la Le Parisien, " maafisa wa kukusanya kodi na maafisa wa Idara inayopambana na uhalifu mkubwa wa kifedha (BRGDF) wamevamia majengo ya kampuni ya Marekani ya Google nchini Ufaransa, kwa msaada wa wanasheria watano wa Ofisi ya taifa mashitaka ya fedha".

Msako huo ulianza Jumanne hii alfajiri saa 05:00 hasa katika makao makuu ya kampuni hiyo mjini Ufaransa. Maafisa wa kodi zaidi ya mia moja na kikosi kinachopambana na uhalifu wa kifedha, wakisaidiwa na wanasheria watano pamoja na wataalam 25 wa kompyuta wamevamia majengo ya kampuni kubwa ya Marekani. Hii ni hatua mpya katika mvutano unaoendelea kati yakampuni ya Google mamlaka ya Ufaransa.

Kufuatia malalamiko ya Bercy tarehe 15 Juni, Ofisi ya taifa ya mashitaka ya fedha ilianzisha uchunguzi wa awali kwa sababu mamlaka ya kodi iliituhumu kampuni ya Google kuwa iliweka mfumo kabambe wa ukwepaji wa kulipa kodi. Serikali ya Ufaransa imekua ikiidai kampuni ya Google Euro bilioni 1.6 ya malimbikizo ya kodi.

"Tunashirikiana na mamlaka ili kujibu maswali yao," msemaji wa kampuni hiyo amesema, akiongeza kuwa Google inatii sheria ya Ufaransa.

Google, ambayo makao yake makuu barani Ulaya yanapatikana nchini Ireland, kama mashirika ya kimataifa mengine, mara kwa mara yanatuhumiwa kujaribu kukwepa kulipa kodi kwa kuwekeza katika nchi ambapo kodi kwa kiasi kikubwa imekua ikiyanufaisha.