Global Witness: Mamia ya wanamazingira waliuawa mwaka 2015

Msitu wa Mau nchini Kenya
Msitu wa Mau nchini Kenya Treasure of Kenya

Watu zaidi ya 185, ambao ni wazawa na wanaharakati wa mazingira, waliuawa mwaka 2015, imesema ripoti ya shirika la waangalizi, Global Witness.

Matangazo ya kibiashara

Shirika hili linasema kuwa idadi hii ni kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa kidunia, ambayo ni karibu na asilimia 60 zaidi ya mwaka 2014, toka taasisi ya Global Witness ianze kuchunguza uhalifu wa aina hii mwaka 2002, na kwamba huenda idadi hii ikawa kubwa zaidi kwakuwa vifo vingi pia havijaripotiwa.

Nchi za Brazil na Ufilipino kwa pamoja zinatajwa kukithiri kwa mauaji ya wazawa na wanaharakati wa mazingira ambao ni robo tatu ya watu wote waliouawa, zikifuatiwa na nchi za Colombia, Peru, Nicaragua na Jamhuri ya Kidemokrasia ya kongo, DRC.

Zaidi ya vifo 40 vilihusishwa na mauaji ya kwenye uwekezaji wa magodi, huku vingine vikiwa vinahusishwa na biashara ya kilimo, uchimbaji mabwawa na uporaji ardhi.