SIASA

Ushindani mkali washuhudiwa katika uchaguzi wa Australia

Kura zikihesabiwa nchini Australia
Kura zikihesabiwa nchini Australia abc.net

Kura zinaendelea kuhesabiwa katika uchaguzi wa wabunge nchini Australia.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa kuna ushindani mkali kati ya chama cha Liberal cha Waziri Mkuu Malcolm Turnbull dhidi ya chama cha upinzani cha Labour kinachoongozwa na Bill Shorten.

Matokeo ya awali yanaonesha kuwa chama cha upinzani kinaongoza kwa viti 67 huku kile cha Liberal kikiwa na viti 66.

Mshindi anastahili kupata angalau viti 75 katika bunge hilo la wabunge 150 ili kuunda serikali.

Wachambuzi wa siasa nchini humo wanasema, hali inavyoonekana kwa sasa itakuwa ni vigumu sana kwa mshindi kupata ushindi wa moja kwa moja.

Raia wa Australia watalazimika kusubiri matokeo ya mwisho siku ya Jumanne juma lijalo.