CUBA- RAUL CASTRO

Mwanamapinduzi wa Cuba Fidel Castro afariki dunia

Raisi wa zamani wa Cuba na mwanamapinduzi Fidel Castro amefariki dunia mjini Havana,mdogo wake Raul Castro ambaye ni raisi wa sasa wa Cuba amethibitisha.

Raisi wa zamani wa Cuba na mwanamapinduzi Fidel Castro
Raisi wa zamani wa Cuba na mwanamapinduzi Fidel Castro Daily Beast
Matangazo ya kibiashara

Akitangaza kupitia televisheni ya taifa Raul Castro amesema amiri jeshi mkuu wa mapinduzi ya Cuba amefariki dunia saa nne na dakika 29 usiku.

Mkongwe huyo wa mapinduzi amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90 ambapo mara ya mwisho alionekana hadharani mwezi August.

Fidel Castro aliongoza Cuba chini ya chama kimoja kwa takribani nusu karne kabla ya kukabidhi madaraka kwa kaka yake Raul mnamo mwaka 2008.

Wafuasi wake wanamsifu kwa kuierejesha Cuba mikononi mwa raia licha ya wainzani wake kumshutumu kwa kushughulikia wapinzani kikatili.
Mnamo mwezi April IFidel Castro alitoa hotuba nadra katika siku za mwisho za chama cha kikomunisti.