MAJI-UNICEF

UNICEF yahofia afya ya Mamilioni ya watoto kutokana na uhaba wa maji safi

Nembo ya UNICEF
Nembo ya UNICEF UNICEF

Dunia inapoadhimisha siku ya maji duniani, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maswala ya watoto la UNICEF, linaonya kuwa zaidi ya watoto Milioni 600 katika maeneo mbalimbali duniani, wataendelea kukosa maji safi ya kunywa na matumizi.

Matangazo ya kibiashara

Inakadiriwa kuwa hali hii huenda itaendelea kufikia mwaka 2040 ikiwa hatua za dharura hazitachukuliwa.

Watalaam wamekuwa wakionya kuwa huenda kukawa na uhaba wa maji safi ya kunywa katika miaka ijayo ikiwa hatua za dharura na za muda mrefu hazitachukuliwa.

UNICEF inasisitiza kuwa, hatua hizo zinastahili kuchukuliwa haraka ili kuwasaidia watu wanaopitia changamoto hii.

Mabadiliko ya hali ya hewa ni sababu mojawapo inayoelezwa kuwa inachangia uhaba wa maji safi huku waathiriwa wakiwa ni watoto.

Ukosefu wa bidhaa hiyo muhimu umesababisha watu wengi wakiwemo watoto kutumia maji safi na kusababisha ugonjwa wa kipindupindu na magonjwa mengine ya kuharisha.

Mataifa 36 duniani, hasa Afghanistan, Somalia, Nigeria na Sudan Kusini yameendelea kukabiliwa na ukosefu wa maji safi ya kunywa na matumizi mengine.

“Mamilioni ya watoto wanakosa maji safi ya kunywa hali inayoendelea kuhatarisha afya zao,” amesema Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF Anthony Lake.