PASAKA-WAKIRISTO

Wakristo waadhimisha Pasaka, huku Papa Francis akitaka vita nchini Syria kukomeshwa

Papa Francis akiongoza ibada ya Pasaka Aprili 16 2017 mjini Vatican
Papa Francis akiongoza ibada ya Pasaka Aprili 16 2017 mjini Vatican REUTERS

Wakiristo kote duniani wamekuwa wakiadhimisha siku ya pasaka huku wengi wakifurika Makanisani na maeneo mengine ya kuabudu.

Matangazo ya kibiashara

Ni kumbukumbuku ya kufufuka kwa Mwokozi Yesu Kristo wanayeamini kuwa  baada ya siku tatu kusulubiwa msalabani.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis, ameongoza ibada mjini Vatican na kutumia siku hii kutoa wito wa kumalizika kwa vita nchini Syria.

Amesisitiza umuhimu na haja ya Jumuiya ya Kimataifa kujitoa ili kuzuia mauaji na mateso ya raia wasiokuwa na hatia katika nchi hiyo.

Mjini Jerusalem nchini Israeli, melefu walijitokeza wakiwemo watalii kutoka nchi mbalimbali kuadhimisha siku hii muhimu.

Jijini Cairo nchini Misri, Wakiristo wa dhahebu la Coptic wameadhimisha siku hii chini ya ulinzi mkali baada ya kushambuliwa kwa makanisa mawili Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 45. Kundi la Islamic State lilidai kuhusika.

Polisi na wanajeshi wameonekana wakipiga doria katika jiji hilo huku wakizingira Makanisa.

Kutokana na tukio hilo, serikali ya Misri imetangaza miezi mitatu ya hali ya hatari na kuagiza jeshi kulinda maeneo muhimu nchini humo.