DUNIA-UHALIFU

Uchunguzi wafanyika kuwapata waliotekeleza uhalifu wa mtandao

Mfano wa namna uhalifu wa mtandao unavyofanyika
Mfano wa namna uhalifu wa mtandao unavyofanyika REUTERS/Kacper Pempel/Illustration

Serikali mbalimbali duniani na watalaam wa maswala ya Kompyuta wanachunguza shambulizi la mitandaoni lililoathiri mataifa 150 kuanzia siku ya Ijumaa wiki iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Kampuni ya Microsoft inasema kilichotokea ni funzo na kifungua macho kwa mataifa mbalimbali na hivyo kuna umuhimu wa kubadilisha na kuimarisha mifumo yake.

Watalaam wanaohusika na usalama wa kompyuta wanasema kuwa zaidi ya kompyuta 200,000 zimeathirika na kuwasababishia hasara maelfu ya watu ambao wamerejea kazini siku ya Jumatatu.

Uvamizi huu umeathiri shughili kwenye benki, hospitali na mashirika mbambali ya serikali.

Rais wa Urusi Vladimir Putin amejitokeza na kukanusha madai ya nchi yake kuhusika na uvamizi huo na badala yake kuishutumu Marekani kwa kupanga tukio hilo.

Nchini China, maelfu ya kompyuta ziliiathirika na uvamizi huu uliolenga zaidi ya taasisi 30,000.

Mashirika ya Marekani ya kusafirisha vifurushi ya FedEx, kampuni ya kutengeneza magari ya Ulaya, mashirika ya simu ya Uhispania kama vile Telefonica, mfumo wa afya wa Uingereza na mtandao wa usafiri wa reli wa Ujerumani uliathirika na uvamizi huu. Bonyeza hapa kusoma zaidi.

Hii ndio mara ya kwanza kushuhudiwa kwa uvamizi mkubwa wa mitandaoni katika miaka ya hivi karibuni.