ITALIA-MAREKANI

Viongozi wa G7 wahitimisha kongamano kwa mgawanyiko kuhusu mkataba wa Paris

Rais wa Marekani na baadhi ya viongozi wa G7 27 May 2017.
Rais wa Marekani na baadhi ya viongozi wa G7 27 May 2017. REUTERS/Alessandro Bianchi

Viongozi wa G7 jana Jumamosi wamehitimisha mkutano wao wa kila mwaka huku mvutano ambao haujawahi kushuhudiwa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi ukidhihirika baada ya Rais wa Marekani Donald Trump akijizuia kuamua katika mkutano huo kuhusu nchi yake kukubaliana na mpango wa kupunguza hewa ya ukaa duniani

Matangazo ya kibiashara

Trump aliyeondoka Sicily hapo jana bila kutekeleza desturi ya kuzungumza na wanahabari kama hitimisho la mkutano, aliandika katika ukurasa wake wa twitter kuwa atafanya uamuzi wiki ijayo kuhusu kama Marekani itafuata makubaliano ya Paris ya mwaka 2015 kuhusu kupunguza hewa ya ukaa duniani au la.

Washirika wa Marekani wameelezea malalamiko yao dhidi ya kushindwa kwa rais Trump kukubaliana na mpango huo wenye lengo la kudhibiti ongezeko la joto duniani.

Hakuna maoni zaidi yanayotarajiwa kutoka kwa rais wa Marekani, ambaye amerejea nyumbani hiyo jana bila kufanya desturi ya kuhitimisha mikutano kwa kuzungumza na wanahabari.