UNHCR-WAKIMBIZI

Dunia inaadhimisha siku ya Kimataifa ya wakimbizi

Wakimbizi wa Syria nchini Lebanon
Wakimbizi wa Syria nchini Lebanon Reuters/Aziz Taher

Dunia leo inaadhimisha siku ya wakimbizi.

Matangazo ya kibiashara

Siku hii hutumiwa  kuwatia moyo Mamilioni ya wakimbizi, waliokimbia makwao na kutafakari maisha magumu na changamoto mbalimbali wanazopitia ili kujikimu maishani.

Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia wakimbizi UNHCR, imesema idadi ya wakimbizi kote duniani umeongezeka na kufikia Milioni 65.6.

Wakimbizi wengi wametoka katika nchi ya Syria, Afganistan na Sudan Kusini huku Umoja wa Mataifa ukisema unahitaji Dola Bilioni 7.7 kuwaisaidia wakimbizi.

Soma pia makala haya.Bonyeza.

Miongoni mwa wakimbizi hao ni 400,000 kutoka nchini Burundi waliokimbia nchi hiyo kwa sababu za kisiasa.

Hata hivyo serikali ya rais Pierre Nkurunziza imekuwa ikidai kuwa nchi hiyo ina usalama lakini watu wameendelea kukimbilia nchi jirani za Tanzania, Rwanda na Jmahuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Maeneo yaliyo na wakimbizi wengi ni kutoka barani Afrika, Mashariki ya Kati na barani Asia.

Nchi wanazotokea idadi kubwa ya wakimbizi:

Syria: Zaidi ya Milioni 5.5
Afghanistan: Milioni 2.5
Sudan Kusini: Milioni 1.4

Mataifa yepi yanaongoza kuwapa hifadhi wakimbizi ?

Uturuki : Milioni 2.9
Pakistan: Milioni 1.4
Lebanon: Milioni 1
Iran: 979,4000
Uganda: 940,800
Ethiopia: 791,600