KANISA KATOLIKI

Kadinali Pell akanusha madai ya kuhusika katika unyanyasaji wa kingono

Kadinali George Pell
Kadinali George Pell sbs.com.au.news

Kadinali George Pell mshauri wa kiuchumi wa Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis, amesema atarejea nyumbani nchini Australia kupambana na madai ya kuhusika katika visa vya unyanyasaji wa ngono dhidi ya watoto.

Matangazo ya kibiashara

Licha ya madai hayo mazito yanayomkabili Kadinali Pell, ameyakanusha vikali.

Papa Francis amemuunga mkono na hajamwambia ajiuzulu.

Kadinali huyo amesema madai hayo yanalenga kumchafulia jina.

Aidha, amesema kuwa baada ya kufika Mahakamani tarehe 18 mwezi Julai, ukweli utabainika na kulisafisha jina lake ili arejee kazini mjini Vatica.

Polisi nchini Australia wamesema kuwa Kadinali huyo amepatikana na kosa la kuhusika na visa vya kihistoria vya unyansaji wa kingono lakini hawakutoa maelezo ya kina.

Kadinali Pell anatuhumiwa kuhusika na visa hivyo wakati alipokuwa Askofu Mkuu wa Sydney mwaka 2002.