MKUTANO WA G20

Viongozi wa G20 waamua mkataba wa mabadiliko ya hali ya hewa ni lazima utekelezwe

Viongozi wa G20 wakiwa katika mkutano wa mjini Hamburg Julai 8 2017
Viongozi wa G20 wakiwa katika mkutano wa mjini Hamburg Julai 8 2017 REUTERS/Patrik STOLLARZ/Pool

Viongozi kutoka tajiri duniani ya G 20, wamekubaliana kutekeleza kikamilifu mkataba wa mwaka 2015 uliofikiwa jijini Paris nchini Ufaransa mwaka 2015, kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Matangazo ya kibiashara

Imekubaliwa kuwa Marekani licha ya kujiondoa kwenye mkataba huo itahakikisha inasaidia utekelezwaji wa mkataba huo na kuyasaidia mataifa mengine kuzalisha na kutumia nishati safi isiyochafua hali ya hewa.

Akisoma taarifa ya mwisho ya mkutano huo wa siku mbili uliomalizika siku ya Jumamosi mjini Hamburg nchini Ujerumani, Kansela Angela Merkel amesema uamuzi wa kuutekeleza mkataba huo hauwezi kubadilishwa kabisa.

Aidha, amesisitiza kuwa mataifa 19 yametambua na kuheshimu uamuzi wa Marekani kujiondoa  katika mkataba huo.

Kuhusu biashara, viongozi hao wamekubaliana kusawazisha biashara ndani ya mataifa hayo 20.