Pata taarifa kuu
SAUDI ARABIA-YEMENI-USALAMA

Wanajeshi wa Saudi Arabia wadhibiti Uwanja wa ndege nchini Yemen

Wanajeshi wa Saudi Arabia wakitekeleza oparesheni katika Uwanja wa ndege wa Hudaida June 15, 2018
Wanajeshi wa Saudi Arabia wakitekeleza oparesheni katika Uwanja wa ndege wa Hudaida June 15, 2018 AFP
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 1

Wanajeshi wa Saudi Arabia wakisaidiana na wale kutoka nchi ya Falme za Kiarabu, wamefanikiwa kudhibiti uwanja wa ndege wa Hudaida nchini Yemen baada ya kuwashinda waasi wa Kihouthi.

Matangazo ya kibiashara

Licha ya taarifa hiyo kutoka kwa jeshi la Saudi Arabia, makabiliano makali yameendelea kushuhudiwa kati ya wanajeshi hao na waasi.

Hata hivyo, waasi hao hawajasema iwapo wameondolewa katika ngome yao.

Mapiagano yamekuwa yakiendelea katika mji huyo wa pwani tangu katikati ya wiki hii na watu zaidi ya 30 wameuawa wengi wao wakiwa waasi wa Kihouthi.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa, amewasili nchini humo kwa lengo la kuzungumza na pande zote ili kuacha mapigano kwa sababu bandari ya Hudaida ndio inayotegemewa kuingiza misaada ya kibinadamu kuwasadia waathiriwa wa mzozo huo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.