KOREA KASKAZINI-MAREKANI-UN

Korea Kaskazini yaishtumu Marekani kwa kutoivumilia

Korea Kaskazini inasema Marekani inaonesha, haina uvumilivu kuhusu harakati zake za kuachana kabisa na mradi wake wa nyuklia wa kutengeneza silaha za maangamizi. 

Kiongozi wa Korea Kaskazini  Kim Jpng Un akizuru moja ya eneo la kutengeza silaha za nyuklia
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jpng Un akizuru moja ya eneo la kutengeza silaha za nyuklia Reuters
Matangazo ya kibiashara

Tuhma hizi za Pyongyang zimekuja baada ya Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani  Mike Pompeo kusisitiza kuendelea kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini.

Kauli ya Pompeo imekuja baada ya ripoti ya watalaam wa Umoja wa Mataifa kuonesha kuwa, Korea Kaskazini inaendeleza mradi huo licha ya kuwekewa vikwazo.

Ripoti hii imekuja baada ya ripoti nyingine kutolewa na kuchapishwa katika Gazeti la Washington Post nchini Marekani, kuhusu mradi huo wa Korea Kaskazini.

Yote haya yanakuja licha ya kuwepo kwa mkutano wa kihistoria kati ya rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskaizni Kim Jong un mwezi Juni nchini Sinapore na Pyongyang, kukubali kuachana kabisa na mradi huo kwa ajili ya amani ya dunia.