UN-KOFI ANNAN

Dr. Kofi Annan aaga dunia akiwa na umri wa miaka 80

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa (UN) Dr. Kofi Annan
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa (UN) Dr. Kofi Annan ®Maxwells/Handout via REUTERS

Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa (UN) Dr. Kofi Annan ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 80.

Matangazo ya kibiashara

“Amefariki akiwa amezungukwa na familia yake  mkewe, Nane na watoto wake Ama, Kojo na Nina," Imesema taarifa ya Mfuko wa Dr. Kofi Annan (Kofi Annan Foundation)

Atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa akiwa katibu mkuu wa umoja wa Mataifa kutoka mwaka 1997 hadi 2007 na pia kuwa msuluhishi wa mizozo mbalimbali ya kisiasa duniani.

Mwaka 2007 alikuwa miongoni mwa wanadiploasia mashuhuri duniani walioongoza jitihada za kuleta utulivu nchini Kenya baada ya machafuko ya uchaguzi wa 2007

Baada ya kumaliza muda wake kama katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 2007 aliteuliwa kuwa mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Syria.

Wakosoaji hata hivyo wanasema akiwa katibu mkuu wa UN alishindwa kuchukua hatua baada ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda yaliyotokea mwaka 1994.