VITA-DUNIA-UFARANSA-MAREKANI-URUSI

Maadhimisho ya miaka 100 kukumbuka kumalizika kwa vita vya 1 vya dunia yaanza Ufaransa

Mfano wa eneo la vita duniani
Mfano wa eneo la vita duniani REUTERS/Maxim Shemetov

Maadhimisho ya wiki moja, kukumbuka kumalizika kwa vita vya kwanza vya dunia, miaka 100 iliyopita, inaanza kusherehekewa nchini Ufaransa.

Matangazo ya kibiashara

Jumapili ijayo, viongozi wa dunia wapatao 80, wakiongozwa na rais wa Marekani Donald Trump, rais wa Urusi Vladimir Putin miongoni mwa wengine, watakutana jijini Paris kuadhimisha siku hii.

Usalama umeimarishwa kote nchini Ufaransa, wakati huu maadhimisho haya yanapofanyika kwa sababu nchi hiyo imeendelea kupokea vitisho kutoka kwa magaidi katika siku za hivi karibuni.

Kuelekea tarehe 11, rais Emmanuel Macron anatarajia kuanza ziara kote nchini Ufaransa kutembelea maeneo ambayo wanajeshi waliokuwa wanapigana katika vita hivyo, walifia.

Vita hivyo vilianza tarehe 28 mwezi Julai mwaka 1914 na kumalizika tarehe 11 mwezi Novemba 11 mwaka 1918, baada ya kudumu kwa miaka minne.

Ni vita vilivyoshuhudiwa barani Ulaya, Afrika, Mashariki ya Kati, China na Amerika Kusini na Kaskazini.

Kati ya watu Milioni 50-100 walipoteza maisha katika vita hivyo vilivyoanzia barani Ulaya.