WHO-UKIMWI-DUNIA-AFRIKA

Siku ya Ukimwi duniani, watu wahimizwa kwenda kupima

Siku ya Ukimwo duniani
Siku ya Ukimwo duniani Hiv.gov

Dunia inaadhimisha siku ya Ukimwi. Haya ni maadhimisho ya 30. Ni siku inayotumiwa na wanaharakati na wakuu wa nchi, kutoa elimu kuhusu namna ya kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi, kupiga vita unyanyapaa na kuhimiza watu kwenda kufanya vipimo ili kufahamu hali zao.

Matangazo ya kibiashara

Shirika la afya duniani WHO linasema, watu Milioni 37 duniani, wanaishi na maambukizi ya ukimwi huku vijana wakiendelea kuwa hatarini zaidi kuambukizwa hasa barani Afrika.

Watu wengine Milioni 22 walioambukizwa, wanatumia dawa ya AVR ambayo imesaidia watu wengi sana kuendelea kuishi.

Maadhimisho haya yamekuwa yakiadhimishwa tangu mwaka 1988, lengo kubwa likiwa ni kutoa elimu kuhusu namna ya kuepuka ugonjwa huu.

Woga, unyanyapaa na kupuuza ni mambo ambayo yanaendelea kuitesa dunia katika mapambano ya ugonjwa huu ambao umesababisha vifo vya Mamilioni ya watu tangu miaka 1980.

Maambukizi mapya yanawaathiri idadi kubwa ya vijana walio na umri wa kati ya miaka 15-25. Katika vijana watano, watatu ni vijana wa kike.

Uchunguzi wa WHO umebaini kuwa, asilimia 71 ya maambukizi mapya yanatokea barani Afrika, hasa eneo la Afrika Mashariki na Kusini mwa bara hilo.

Ili kupunguza maambukizi kwa vijana, watalaam wanapendekeza kuwa, wasichana wapate nafasi ya kwenda shuleni kwa wingi, uzuiaji wa dhuluma dhidi ya wanawake lakini pia kuongezeka kwa huduma ili kutolewa kwa elimu ya afya ya uzazi.

Nini kifanyike ?

Kauli mbinu ya maadhimisho ya mwaka 2018, ni kufahamu hali yako, ni muhimu kwa kupima.

Takwimu za WHO zinaonesha kuwa mtu mmoja kati ya wanne, hawafahamu hali yao ya HIV.

Kuongeza uhamasishaji, WHO inapendekeza kuwepo kwa mashine binafsi ya kufanya vipimo, ambavyo vilianza kutumiwa mwaka 2016.

Watu walioambukizwa pia wapo kwenye hatari kubwa ya kusumbuliwa na magonjwa mengine kaa TB na Hepatitis, na mtu mmoja kati ya watu walio na HIV hufariki dunia kwa sababu ya TB.

Mtu anaweza kupata vipi HIV ?

  • Kushiriki ngono na mtu aliyeambukizwa bila kutumia kinga.
  • Kutumia sindanio au kitu chenye ncha kali kilichotumiwa na mtu aiyeambukizwa, hasa wale wanaojidunga dawa za kulevya.
  • Kutoka kwa mama, kwenda kwa mtoto hasa kwa kumyonyesha. Mama mwenye HIV hastahili kumyonyesha mtoto.
  • Kuingiziwa damu, iliyoambukizwa virusi vya HIV.

Kujikinga na HIV

  • Kutumia kinga, mpira wa Condom
  • Kuepuka ngono, hasa kwa vijana hadi kuoa au kulewa
  • Ukiolewa kuwa mwaminifu kwa mwezi wako.