HALI YA HEWA-POLANDA-PARIS-UN-2020

Mkataba wa kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa kuanza kutekelezwa mwaka 2020

Uharibifu wa hali ya hewa duniani
Uharibifu wa hali ya hewa duniani ©REUTERS/Kacper Pempel

Wajumbe kutoka mataifa zaidi ya 200 ambao wamekuwa wakikutana nchini Poland, kujadili namna ya kutekeleza mkataba wa mabadiliko ya hali ya hewa uliokubaliwa jijini Paris nchini Ufaransa mwaka 2015, wamekubaliana namna ya kuanza kuutekeleza.

Matangazo ya kibiashara

Makubaliano haya yamekuja, baada ya mazungumzo ya wiki mbili kuthathmini mbinu za kuhakikisha kuwa, ongezeko la joto duniani linapunguzwa na halizidi senti gredi mbili.

Aidha, imekubaliwa kuwa utekelezwaji wa mkataba huu utaanza mwaka 2020 ili kufikia lengo la kupunguza hewa chafu ya Carbon.

Aidha, kufikia mwaka 2030, mkataba huo ukitekelezwa kikamilifu hewa chafu ya Carbon inatarajiwa kushuka hadi senti gredi 1.5.

Hata hivyo, mataifa ya Marekani, Saudi Arabia na Kuwait walipinga namna mkataba huo ulivyokuwa umewasilishwa hapo awali, ikabidi ufanyiwe mabadiliko ya maneno.

Kipindi chote cha mazungumzo hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress alishiriki katika vikao hivyo katika jiji la Katowice, amesisitiza kuwa kazi kubwa ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani, ndio imeanza.