UFARANSA-MAANDAMANO-SIASA-KODI

Polisi nchini Ufaransa yajiandaa kukabiliana na waandamanaji wanaopinga sera za rais Macron

Rais Emmanuel Macron anakabiliwa na mfululizo wa maandamano yanayopinga sera za serikali yake
Rais Emmanuel Macron anakabiliwa na mfululizo wa maandamano yanayopinga sera za serikali yake twitter/bloomberg

Polisi jijini Paris hii leo wanajiandaa kukabiliana na mamia ya waandamanaji waliopanga kujitokeza kwenye viunga vya miji mbalimbali nchini humo kuadhimisha siku ya Wafanyakazi na kupinga sera za rais Emmanuel Macron.

Matangazo ya kibiashara

Juma lililopita waandaaji wa vizibao vya njano waliitisha maandamano makubwa hivi leo, maandamano ambayo Serikali imesema haitakuwa na huruma na waandamanaji ambao watashiriki kufanya vurugu.

Mashirikisho ya wafanyakazi nchini Ufaransa pia yamewataka raia kujitokeza kwa wingi hii leo kushinikiza kuboreshwa kwa mazingira ya kazi na maslahi.