VENEZUELA-SIASA-NICOLAS MADURO-JUAN GUAIDO

Polisi yakabiliana na waandamanaji nchini Venezuela

Mji wa Caracas unashuhudia maandamano tangu ulipozuka mgogoro nchini Venezuela
Mji wa Caracas unashuhudia maandamano tangu ulipozuka mgogoro nchini Venezuela REUTERS/Carlos Garcia

Waandamanaji nchini Venezuela wamekabiliana na polisi kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Caracas, wakiitikia wito wa kinara wa upinzani Juan Guaido aliyetaka wanajeshi zaidi wamuunge mkono kumuondoa madarakani rais Nicolas Maduro.

Matangazo ya kibiashara

Katika kile kinachoonekana na mapinduzi yanayopangwa na Guaido kwa kuwashawishi wanajeshi zaidi kumuunga mkono, kumeshuhudiwa maandamano ya hapo jana yakigeuka kuwa vurugu.

Usiku wa kuamkia leo rais Nicolas Maduro kupitia njia ya televisheni, alizungukwa na maofisa wa juu wa jeshi kuonesha bado anaungwa mkono huku akiwasifu kwa kutomsaliti kama ambavyo baadhi wamefanya.

Rais Maduro amesema vyombo vya sheria vitahakikisha vinawashughulikia wale wote aliosema wamevunja katika kwa kushiriki maandamano haramu na kupanga njama za kuipindua Serikali yake.