MAREKANI-IRAN-VITA-SIASA

Trump: Iran isijaribu kupigana nasi, tutaimaliza

Rais wa DRC  Donald Trump
Rais wa DRC Donald Trump MANDEL NGAN / AFP

Rais wa Marekani Donald Trump ameionya Iran kuwa ikitaka mapambano kwa kushambulia maslahi ya Marekani huo ndio utakaokuwa mwisho wa nchi hiyo ya Mashariki ya Kati duniani.

Matangazo ya kibiashara

Kupitia ukurasa wake Twitter, rais Trump ameonya kuwa iwapo Iran inataka kupigana basi huo utakuwa mwisho ramsi wa jamuhuri hiyo ya Kiislamu.

Mvutano kati ya Washington na Tehran umeongezeka wakati huu Marekani ikipeleka wanajeshi wake katika eneo la ghuba ya kiarabu kufuatia kile ilichookiita ni tishio la kiusalama kutoka Tehran.

Utawala wa Trump umeamuru kuwa  wafanyakazi wasiokuwa wa kidiplomasia kuondoka nchini Iraq, kufuatia vitisho kutoka kwa vikundi vinavyomiliki silaha nchini Iraq vinavyoungwa.

Jumapili iliyopita, roketi  ililenga katika ofisi za serikali ya Baghdad na balozi ikiwa ni pamoja na walinda amani wa Marekani.

Haikuwa wazi wazi nani alihusika na shambulizi hilo.

Marekani pia imekuwa katika mstari wa mbele kupinga mkataba wa Kimataifa wa nyuklia uliotiwa saini mwaka 2015, na badala yake kuendelea kuiwekea Tehran vikwazo.

Uongozi wa Iran unasema hauna mpango wala haja ya kupigana na Marekani au kuanzisha vita.