UFARANSA-VITA-MAREKANI-UINGEREZA

Viongozi wa dunia wakutana Kaskazini mwa Ufaransa kuadhimisha miaka 75 baada ya D-Day

Viongozi wa dunia, wamekuwa Kaskazini mwa Ufaransa kuadhimisha miaka 75 tangu kukamilika kwa vita vya dunia, wakati muungano wa wanajeshi kutoka mataifa mbalimbali yakiongozwa na Marekani na Uingereza walipokusanyika kukabiliana na wanajeshi wa Ujerumani Kaskazini mwa Ufaransa. 

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (Kulia) na Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May (Kushoto) wakiwasili katika eneo la maadhimisho ya D-Day Juni 6 2019
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (Kulia) na Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May (Kushoto) wakiwasili katika eneo la maadhimisho ya D-Day Juni 6 2019 www.rfi.fr
Matangazo ya kibiashara

Wakiongozwa na rais Emmanuel Macron, mwenzake wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May, wameadhimisha siku hii na kusema kauli yao ni moja tu, kusema asante kwa wanajeshi walioweka maisha yao hatarini, kulikomboa bara la Ulaya na kufanya watu kuwa huru.

Siku ya Jumatano, viongozi wa mataifa mbalimbali walikutana nchini Uingereza kuadhimisha pia siku hiyo ambayo muungano wa kijeshi ulipovamia Kaskazini mwa Ufaransa, kipindi cha vita kuu ya pili ya dunia, maarufu kama D-Day.

Muungano huo wa kijeshi ulisaidia kuikomboa Ujerumani kutoka kwa wapiganaji wa Kinazi, wakiongozwa na Dikteta Adolf Hitler.

Hitler, alisababisha kuanza kwa vita vya pili vya duniani, vilivyokuwa vibaya sana katika historia ya vita duniani, baada ya wanajeshi wake kuvamia nchi ya Poland mwaka 1939.