Pata taarifa kuu
WHO-CHANJO-AFYA-SIASA

Watalaam wa afya waonya kuwa watu hawaamini chanjo

Wataalam wa afya
Wataalam wa afya RIZWAN TABASSUM / AFP

Watalaam wa afya duniani wanaonya kuwa kuendelea kupuuza chanjo mbalimbali, kunarudisha nyuma jitihada za kutokomeza magonjwa mbalimbali ya kuambukiza.

Matangazo ya kibiashara

Utafiti wa taasisi ya Wellcome Trust yenye makao yake jijini London nchini Uingereza,inaonesha kuwa baada ya kuwahoji watu zaidi ya 140,000 katika zaidi ya mataifa 140, imebainika kuwa watu hawaamini tena chanjo.

Utafiti huu unakuja wakati huu ambao watalaam wakisisitiza kuwa kutolewa kwa chanjo kumewasaidia mabilioni ya watu duniani.

Hata hivyo, wanaonya kuwa ugonjwa kama surua haukatokomezwa kabisa duniani kwa sababu ya watu kutofahamishwa vema kuhusu chanjo.

Daktari Ann Lindstrand, mtalaam wa chanjo kutoka Shirika la afya duniani WHO anasema kuwa hali inayoshuhudiwa ni hatari sana kuonya kuwa iwapo hali itaendelea kuwa hivi, huenda magonjwa hatari yakarejea tena.

Watalaam wa afya wamefanikiwa kutokomeza magonjwa kama Polio na ukoma katika miaka kadhaa iliyopita.

Barani Afrika, kuna baadhi ya madhehebu hayaamini katika chanjo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.