DUNIA-HALI YA HEWA-SIASA-MAANDAMANO

Maandamano makubwa duniani kuhamasisha makabiliano dhidi ya mabadiliko ya hewa

Waandamanaji wa mazingira barani Asia
Waandamanaji wa mazingira barani Asia REUTERS/Wolfgang Rattay

Maandamano makubwa yanafanyika kote duniani  kuhamasisha viongozi wa dunia kufanya vya kutosha kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya waandamanaji wameonekana katika miji mbalimbali barani Asia, wengi wao wakiwa ni wanafunzi, wakiwa na ujumbe kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yanaiharibu dunia.

Baadhi ya waandamanaji nao wamebeba mabango yanayosomeka, “Hatuna dunia nyingine”.

Haya ni maandamano yanayofanyika kuelekea mkutano wa Umoja wa Mataifa wiki ijayo, jijini New York nchini Marekani, kujadili mbinu za namna ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Ongezeko la kiwango cha maji baharini pia kinahatarisha kusombwa kwa visiwa hasa nchini New Zealand, Australia na Thailand.

Makampuni mengi yamefunga ili kuwaruhusu watu wengi kwenda kushiriki katika maandamano haya.

Mwaka 2015, viongozi wa dunia walikutana jijini Paris na kukubaliana kuja na mkataba wa kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa kuhadkikisha kuwa, kiwango cha joto hakivuki Senti dregi mbili lakini pia kuondoa kabisa gesi aina ya Carbon kufikia mwaka 2030.